The House of Favourite Newspapers

Wolper Achomoa Kuwa Mbabe Penzini

0

MUIGIZAJI Jacqueline Wolper amesema kuwa yeye sio mbabe kwenye mapenzi kama ambavyo watu wengi wanavyodhani.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake, alisema kwamba baadhi ya mashabiki wake huwa wanadhani anaachana na wapenzi wake kwa sababu ya ubabe, jambo ambalo sio kweli.

“Kuna kitu watu hawakijui kutoka kwangu, mimi linapofika suala la mapenzi, huwa sina ujanja kabisa, nakuwa mpole, natulia na kumheshimu sana huyo mtu ninaye kuwa naye kwa wakati huo, sema tu kuna mambo huwa yanaingiliana, ndipo mwisho wa siku inatokea tumeachana, lakini sio kwa sababu ya ubabe,” alisema Wolper.

 

Mrembo huyo alizua gumzo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kudaiwa kuchumbiwa na Chid Designs ambaye waliachana ndani ya siku kadhaa.

Leave A Reply