The House of Favourite Newspapers

Msigwa Ni Miongoni Mwa Watu Wachache Ambao Wanatambua Na Kueshimu Kazi Ya Dkt. Samia – Makonda

0

Mwenezi Paul Makonda amebainisha kuwa moja kati ya Watu wa vyama vya watoa taarifa ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Ndugu. Peter Msigwa ni mmoja kati ya watu wachache kutoka kwa wapinzani ambaye wanatambua na kueshimu kazi za watu wengine.

Makonda amebainisha hilo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Iringa Mjini.

“Mch. Peter Msigwa ni miongonk mwa watu wachache ambao huwa wanatambua na kueshimu kazi za watu wengine, mimi shida yangu ni moja huwa nasema kile ninachokiamini”

“Rais Samia alipokuwa kwenye kampeni ya Tanzania The Royal Tour katika kuutangaza utalii wa nchi yetu, Peter Msigwa alijitokeza na kusema hili ni jambo jema na la kuungwa mkono”

“Naamini hata kule CHADEMA alipokuwa ni ilikuwa njia ya kutafuta maisha tu maana hafanani nao kabisa, sisi CCM tunamla nafasi kama akiona kule maisha hayaendi basi tutampa kiwanja afungue kanisa na kuendeleza huduma ya kumtumikia Mungu”

Ndugu. Paul Makonda
Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa

📍Iringa Mjini
🗓️ 8 Februari, 2024

Leave A Reply