The House of Favourite Newspapers

Mzee Miaka 76 Adai Alipigwa Risasi Na Polisi Aibua Mazito – Amuomba Rais Samia -Video

0

Mzee Abdallah Ngombo (76), mkazi wa Mkuranga mkoani Pwani ambaye anadai kupigwa risasi na kuvunjwa mguu na askari wa Jeshi la Polisi, Kituo cha Mkuranga amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata lake ili haki itendeke.

Mzee Ngombo ameeleza kwamba tukio hilo limemsababishia ulemavu wa kudumu kwani mguu haujapona mpaka sasa na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya askari waliomtendea ukatili huo wakimtuhumu kuwa ni jambazi.

Mzee Ngombo amesema mwaka mmoja umepita bila ya hatua zozote kuchukuliwa licha ya jeshi la polisi kupitia msemaji wake kutoa taarifa ya kulichunguza tukio hilo na mpaka sasa hawajapewa mrejesho wowote, huku akiteseka kwa kutembelea magongo.

Ameeleza kuwa wamefuatilia suala hilo mpaka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani lakini hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa.

Leave A Reply