The House of Favourite Newspapers

Msolla Aliamsha Dude Yanga, Ataka CV

Dk Mshindo Msolla

SIKU chache tangu aanze kufanya kazi ndani ya Klabu ya Yanga, mwenyekiti mpya klabuni hapo, Dk Mshindo Msolla amewataka watendaji wote wanaofanya kazi ndani ya klabu hiyo kuwasilisha wasifu (CV) wao kwa ajili ya ukaguzi.

 

Msolla alichaguliwa hivi karibuni kuwa mwenyekiti mpya wa Yanga baada ya klabu hiyo kutokuwa na viongozi wa juu wa kuteuliwa kwa muda mrefu kufuatia wale waliokuwepo awali kujiuzulu katika nyakati tofauti.

 

Kiongozi huyo amedai kuwa amejipanga kuleta mabadiliko klabuni hapo, ili iweze kuwa ya kisasa zaidi kwa kuboresha kila idara.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Msolla alisema kuwa anachohitaji hivi sasa ni kuhakikisha watendaji wote wanaofanya kazi ndani ya klabu hiyo wanawasilisha CV kwa ajili ya kuzikagua ili kujua nani anastahili kuendelea kuwepo na nani hastahili.

 

“Kwa sasa tupo katika mchakato wa kujenga taasisi ndani ya klabu yetu ya Yanga, kila mmoja atafanya kazi kulingana na uwezo wake na jinsi CV yake inavyojieleza na si vinginevyo.

 

“Tutawataka wafanyakazi wote kuwasilisha CV zao ili kufanya mchakato upya wa kutoa ajira kwa wote, tunahitaji wafanyakazi wawe na vigezo vinavyotakiwa, tutafanya tathimini ya kila mmoja kujua nani atafaa kuendelea na yupi hastahili, tukiwa na lengo moja tu la kufanya maboresho ndani ya klabu na wasiostahili tutaachana nao,” alisema Msolla.

Stori na Khadija Mngwai na Martha Mboma

Comments are closed.