Msolla Ataja Kirusi Cha Mabadiliko Yanga

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa ugumu wa miundombinu ya kukutana na wanachama nchi nzima ni moja ya kitu kinachofanya mpango wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo yawe ya taratibu.

 

Msolla alisema ishu ya mabadiliko inatakiwa imfikie kila mwanachama ili atoe maoni yake, hivyo ugumu umekuwa kwenye kukusanya maoni hayo kwa mara moja na kuyafanyia maamuzi.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Msolla alisema amekuwa akifanya ziara ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kukutana na viongozi wa matawi na wanachama wa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuchukua maoni yao kwa pamoja kabla ya kukutana na kutoa maamuzi ambazo yatakuwa na tija kwa klabu hiyo.

 

“Watu wamekuwa wakihoji sana kuhusu suala la mabadiliko, wengi wanasema mbona yanachelewa, ukweli ni kwamba miundombinu siyo rafiki, kwa sababu huu mchakato unamhusu kila Mwanayanga.”Kwa sababu kila mwanachama anatakiwa achangie maoni yake juu ya mchakato huu wa mabadiliko, kwa sababu hii ni timu ya wananchi na wanatakiwa kushiriki kwenye kila hatua,” alisema Msolla.

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam

SENZO na INJINIA HERSI Wafunguka, SARPONG kuondoka YANGA, USAJILI wa JOB na FISTON

Toa comment