Msuva aahidi jambo Stars

NYOTA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva, amesema kuwa, wataendelea kupambana katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia kuhakikisha wanafikia malengo.

Kauli ya Msuva imekuja baada ya juzi Jumapili kufunga bao pekee na kuipa ushindi Taifa Stars wa 1-0 ugenini dhidi ya Benin katika mchezo wa Kundi J wa kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Akizungumza na Spoti Xtra, Msuva alisema: “Nafurahi kuona nimeisaidia timu kuibuka na ushindi, kuhusu rekodi ya kufunga mabao mawili muhimu ya ugenini ni juhudi tu na kuhitaji kuisaidia timu. Siwezi kusema nimefanikisha haya nikiwa peke yangu bali ni kwa msaada wa wachezaji wenzangu ambao tumekuwa na lengo moja.

“Malengo yetu ni kufanya vizuri, hakuna mchezaji asiyekuwa na ndoto ya kucheza michuano mikubwa kama Kombe la Dunia, hivyo naamini Mungu yupo pamoja na sisi, tutapambana mpaka hatua ya mwisho.”

Hii ni mara ya pili katika mechi hizo za kufuzu za Kundi J Msuva anafunga bao ugenini akianza dhidi ya DR Congo katika sare ya 1-1.2179
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment