The House of Favourite Newspapers

Msuva Bhana, Eti Mbaraka, Abdulrahman Hawamtishi

0
Mshambuliaji  wa Yanga, Simon Msuva

Stori Musa Mateja | Championi Jumamosi | Habari

SIMON Msuva wa Yanga ana mabao 12 katika Ligi Kuu Bara sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, winga huyo huyo amepiga mkwara akisema hatishwi na kasi ya wafungaji wenzake katika ligi hiyo.

Ukiachana na Abdulrahman, Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar na Shiza Kichuya wa Simba, nao wana mabao 11, yaani moja pungufu ya yale yaliyofungwa na Msuva.

Msuva ameliambia Championi Jumamosi kuwa, hatishwi na kasi ya ufungaji ya wapinzani wake hao isipokuwa yeye anapambana kuhakikisha anafunga zaidi ili kuongeza mabao yake.

Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar.

“Kufunga ni kazi yao, hakuna haja ya kuwaogopa kwani na mimi nitapambana kuhakikisha nafunga kila ninapopata nafasi na si zaidi ya hapo, sina hofu wala hao wafungaji wengine hawanitishi.

“Mchezaji unatakiwa ujiamini kwa kile unachokifanya pia kumuomba Mungu kwa kila hatua mahali popote pale, sasa naamini nitafunga mabao mengi na kuwa mfungaji bora.

Shiza Kichuya wa Simba.

“Katika maisha huwezi kupata kitu kirahisi pasipo kupambana kwa uwezo wote, naamini kila kitu kinawezekana hivyo nitamuomba Mungu anijaalie ili maumivu yanipitie mbali tu,” alisema Msuva.

Leave A Reply