The House of Favourite Newspapers

Msuva: Simba Wakiteleza tu, Wasahau Ubingwa

STORI: NA MUSA MATEJA | CHAMPIONI| DAR ES SALAAM

SAHAU kuhusu matokeo ya jana ya Yanga na Stand United ya Shinyanga katika Ligi Kuu Bara, winga wa timu hiyo, Simon Msuva amesema Simba ikifungwa na Majimaji leo, basi wasahau kuhusu ubingwa msimu huu.

Msuva amewapa tahadhari Simba kwa kusema, endapo mechi yao na Majimaji watapoteza, basi wafute kabisa ndoto za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Yanga kwa sasa ndiyo inayoongoza ligi hiyo kwani kabla ya mechi ya jana ilikuwa na pointi 46 mbele ya Simba yenye 45, halafu nafasi ya tatu ipo Kagera Sugar yenye pointi 37 kisha Azam FC ni ya nne na pointi 34.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Msuva alisema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika kila mchezo wao jambo ambalo litawafanya kuchukua ubingwa kirahisi.

Yanga wakishangilia bao

“Kikosi chetu kipo salama kiasi kwamba tunachowaza sasa ni kuendelea kushinda kila mchezo ili tuweze kutwaa ubingwa kwa mara nyingine tena, tunajua tuko kileleni kwa zaidi ya pointi moja, hatutaki kushuka.

“Simba wameenda kucheza Songea na si rahisi kwao kupata ushindi, ninachoweza kuwaambia ni kwamba wajue kuwa wakizidi kuteleza tu basi safari yao itakuwa imeishia hapo, hawawezi kuwa mabingwa,” alisema Msuva mwenye mabao tisa katika ligi kuu kabla ya mechi ya jana.

Yanga Yaichapa Stand United 4-0 Taifa 2017 “Magoli yote Haya Hapa”

Save

Comments are closed.