The House of Favourite Newspapers

Msuva: Tunawapiga APR kwao

0

Na Omary Mdose
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, amesema wameenda Rwanda kupambana na APR huku wakiamini watarudi na ushindi licha ya wapinzani wao hao kuonekana ni wagumu.

Msuva ambaye tayari yupo Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo huo, alisema hayo kabla ya kutua nchini humo jana asubuhi ambapo watakipiga dhidi ya APR katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Ni kweli tunaenda kupambana na APR, timu ambayo si ya kuibeza, tumejipanga kupambana nao na kuwashinda kwani hilo ndilo lengo letu tulilojiwekea la kutaka kumaliza kazi mapema ili mechi ya marudiano iwe rahisi kwetu.

“Umoja na ushirikiano ndiyo unahitajika kwa sasa ili kufanikisha hili, mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono bila ya kusahau dua zao kwani zina umuhimu wake katika mapambano haya,” alisema Msuva.

Leave A Reply