The House of Favourite Newspapers

Kikongwe afariki dunia

0

Stori:  Mwandishi Wetu, Wikienda
Dar es Salaam: Kikongwe Madina Kiumbe, mkazi wa Mwenge, jijini Dar, aliyezaliwa mwaka 1930, huko Ujiji mkoani Kigoma amefariki dunia hivi karibuni kutokana na ugonjwa wa miguu uliomsumbua kwa muda mrefu na maradhi ya UTI yaliyomsababishia homa kali kiasi cha kupoteza kabisa uwezo wa kula.

Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, mjukuu wa bibi huyo, Arubee Ngaruka alisema bibi huyo aliyeacha watoto wawili, Sittu na Mariam Ngaruka, wajukuu sita na vitukuu tisa, alikuwa na mambo ya kushangaza enzi za uhai wake ambayo si rahisi kuyaona kwa binadamu wengi katika zama hizi.

“Alikuwa ni mtu anayependa kufanya dua muda wote kiasi kwamba mtu yeyote aliyekuwa akienda kwake hatoki bila kufanyiwa dua, alikuwa na moyo wa kutoa na mtu mwenye kumbukumbu mno,” alisema Arubee na kuongeza:
“Bibi Madina, aliyeacha darasa la Madrasa huko kwao Kigoma, alizikwa Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply