visa

Mtibwa kuibeba Yanga mechi za Simba SC

KAMA Mtibwa walichopania kuifanyia Simba wakikifanikisha kwenye mechi zao mbili, wataibeba Yanga kwenye mbio za ubingwa bila kujijua.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema; “Tuna mechi mbili ngumu dhidi ya Simba ambazo tunahitaji kupata matokeo mazuri kama tulivyofanya kwa Yanga tulivyocheza nao pale Morogoro.”

 

“Lakini ukiangalia hata ndugu zetu wameweza kupata matokeo mazuri kwa Simba, baada ya kushinda mechi zote mbili na sisi tutafanya kama walivyofanya Kagera maana wale ni ndugu kabisa nao walikuwa kwenye hatari ya kushuka hivyo lazima tufanye kweli,” alisema Kifaru.

IBRAHIM MUSSA, DAR
Toa comment