Mtibwa Yapewa Timu Ngumu Uganda

KCCA ambayo haijapoteza mchezo kwenye Ligi Kuu ya Uganda msimu huu itacheza na Mtibwa Desemba 15 katika mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.

 

Mechi hiyo itapigwa Kampala kabla ya ku­rudiana Dar es Salaam Desemba 21 ndani ya Uwanja wa Chamazi. KCCA wamecheza mechi tisa za ligi wanaongoza kwa pointi 21 huku Mtibwa ikiwa na pointi 23 wakiwa wamepoteza mechi tano za ligi.

 

KCCA imeanza raundi ya kwanza kutokana na kufanya vizuri kwenye mi­chuano hiyo msimu ulio­pita huku Mtibwa wakifuzu baada ya kuwatoa vibonde Dynamo ya Shelisheli.

 

Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser alisema timu hiyo baada ya kutua Dar es Salaam wanakwenda moja kwa moja kambi kuanza maan­dalizi ya KCCA ambayo wanaiheshimu.

Kama Mtibwa akiwatoa KCCA, watacheza mechi nyingine moja ya mtoano nyumbani na ugenini ili kufuzu hatua ya makundi ya Shirikisho.

 

Mechi hiyo ya mtoano ni dhidi ya timu zilizo­tolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mab­ingwa Afrika.

Toa comment