The House of Favourite Newspapers

Mtoto Akumbwa Na Gonjwa La Ajabu

0
Mtoto Amina Raheem (16) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Zoni, Mbezi jijini Dar.

HUJAFA ujaumbika! Ndiyo maneno unayoweza kusema kutokana na mtoto Amina Raheem (16) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Zoni, Mbezi jijini Dar ambaye anateseka baada ya kukumbwa na gonjwa la ajabu. Akizungumza kwa huzuni baba wa mtoto huyo, Raheem Rashid alisema mwanaye huyo ambaye ni mapacha alizaliwa akiwa mzima lakini miezi mitatu iliyopita alianza kuugua ugonjwa wa ajabu kwani miguu na mikono inakufa ganzi, masikio hayasikii na amepoteza uwezo wa kuona vizuri.

MSIKIE BABA MZAZI “

Mwanangu amezaliwa mzima kabisa na ndiyo alikuwa anamalizia darasa la saba mwaka huu lakini miezi mitatu sasa hajaweza kwenda shule kutokana na miguu kushindwa kutembea kutokana na tatizo la ganzi, masikio hayasikii wala haoni vizuri hata kuongea kwake ni shida,” alisema baba huyo.

Amina Raheem akiwa na baba yake.

ANA WAGOJWA WATATU, UGONJWA WA KUFANANA

Aliendelea kueleza: “Katika familia yangu nina wagonjwa watatu ambao ni huyo mtoto, mama yake na dada wa mtoto huyu, wote wanaumwa ugonjwa unaofanana jambo ambalo nashindwa la kufanya kwani hata uwezo wa kuwapeleka hospitali kwa ajili ya vipimo na matibabu sina.

“Mwanangu huyu baada ya kuugua hivi nilimchukua na kumpeleka kituo kidogo cha afya kilichopo Mbezi mwisho pamoja na mama na dada yake ambapo walipewa dawa, wenzake wakapata nafuu kidogo lakini bado sijapata fedha za kwenda kuwafanyia vipimo kwa kina pamoja na matibabu.

ANAMUOMBA MAMA SAMIA, WATANZANIA

“Nina watoto watano na huyu Amina ndiye aliyekuwa mchangamfu kuliko wengine wote na ana kiu sana ya kusoma lakini ndiyo hivi maradhi yanamsumbua, namuomba Makamu wa Rais, mama Samia Suluhu Hassan anisaidie pamoja na Watanzania wenzangu ili mtoto huyu na wenzake wapate matibabu.

“Nimefika mwisho wa akili zangu jamani, nawaombeni msaada naamini wakipata vipimo na matibabu ya kina watapona kwani hapa nilipo nimekosa fedha kwa ajili ya kuwapeleka kwenye matibabu zaidi, mama yao  ana goita pia ana ugonjwa unaofanana na mtoto huyu pamoja na dada yake wa kupooza na kupoteza uwezo wa kuona,” alisema kwa masikitiko baba huyo. Kwa yeyote aliyeguswa na habari ya mtoto huyu na familia hii anaweza kutuma chochote kwa kutumia simu ya mkononi ya baba yake ambayo ni namba 0715 723 715.

(NA GLADNESS MALLYA,UWAZI)

 

Leave A Reply