The House of Favourite Newspapers

Kafulila: Naunga Mkono Juu Ya Hatua Zinazochukuliwa na Rais Sakata La Escrow (Picha + Video)

0
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini na sasa ni Kada wa Chadema, David Kafulila (kulia) akihojiwa na Mhariri wa Uwazi, Elvan Stambuli leo Global TV Online.

KADA maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), David Kafulila amesema anaunga mkono hatua zote zinazochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli juu vita ya ufisadi uliofanyika ikiwemo sakata la wizi wa fedha za umma, kupitia akaunti ya Tegeta Escrow na madini yanayosafirishwa ndani ya mchanga (makinikia).

Mahojiano yakiendelea

Katika mahojiano maaluma na Global TV Onlin leo jioni, Kafulila ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, ameweka wazi mazingira mengi,  tangu alivyoanza kushughulika na sakata la Escrow bungeni mwaka 2014 hadi namna ambavyo alianza kutishiwa maisha na baadhi ya viongozi wa serikali.

Akifafanua sakata la Escrow

Alisema: “Anachokifanya rais ni sahihi kabisa, kwani ni wazi kwamba Watanzania wengi walijua wanaibiwa lakini kujua kwamba wanaibiwa vipi ilikuwa gizani, lakini rais ameweka wazi amzingira yote na namna ambavyo rasilimali zetu zinachukuliwa kwa mtindo usiokuwa na utaratibu maalum, kwa hiyo binafsi naunga mkono asilimia zote juu ya hatua ambazo rais anazichukua juu ya utetezi wa mali za umma na taifa letu.”

Picha baada ya mahojiano

Kuhusu maisha ya kutishiwa maisha, Kafulila aliongeza; “Kwanza mtakumbuka kwamba wakati nawasilisha hoja bungeni juu ya sakata la Escrow, nilikumbana na vita kali sana, kutokana kwa viongozi wa serikali, akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema ambaye alithubutu kunyanyuka kitini kwake ili aje anipige mezani kwangu, niliposema yeye ni mwizi, baada ya yeye kuniita jina la udhalilishaji la Tumbili.

Akisalimiana na Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.

“Marehemu Samwel Sitta, Dk Mary Nagu na baadhi ya wabunge walimzuia, pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (jina tunalo), alinipigia simu moja kwa moja na kunitishia mambo mengi ya ajabu, pia niliwahi kufuatwa nyumbani na watu waliojitambulisha kama wanausalama, kwa lengo la kunihoji  ambao walinitaka niachane na suala la Escrow kwa madai kwamba mamlaka za juu zinashughulikia, huku umeme ukiwa umekatwa nyumbani kwangu tu.

Akiwa na Mwandishi wa Global Brighton Masalu.

“Kwa kweli mazingira yalikuwa ya namna hiyo, ndoa nayo ilikuwa bado changa hivyo mke wangu (Jesca Kishoa) akawa ananisihi niachane na sakata la Escrow, ilikuwa tabu kwelikweli,” alisema Kafulila.

Habari: Brighton Masalu/ GPL

Leave A Reply