The House of Favourite Newspapers

Mtoto Aliyefanya Mtihani Darasa la 7 Gerezani Afaulu kwa Daraja la Juu – Video

0

KIJANA Kunde Gambija Kilulu (15) ambaye anashikiliwa katika Gereza la Bariadi mkoani Simiyu alikuwa miongoni mwa zaidi ya watahiniwa milioni 1.1 waliofanya mitihani ya darasa la saba na hatimaye kufaulu kwa daraja B.

Wakati wanafunzi wenzake wakifanya mitihani hiyo wakiwa katika mazingira ya kawaida shuleni, kwake ilikuwa tofauti kwa sababu aliifanyia mtihani huo gerezani alikowekwa mahabusu kutokana na tuhuma za mauaji zinazomkabili yeye na baba yake mzazi.

Leave A Reply