The House of Favourite Newspapers

Mtoto Aliyefariki 2017, Apatikana Akiwa Hai, Kaburi Lafukuliwa

0

JESHI la Polisi mkoani Geita limelazimika kufukua kaburi la mtoto aliyefariki dunia katika Hospitali ya wilaya ya Geita kwa ugonjwa upungufu wa damu mwaka 2017 (miaka minne iliyopita) baada ya mtoto huyo kupatikana Kahama mkoani Shinyanga hivi karibuni akiwa hai huku akiwa amekatwa ulimi wake na hivyo kushindwa kuzungumza.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishana msaidizi Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Leonard Morisha alifariki Juni 27, 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama Oktoba 2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua Desemba 12, mwaka huu.

 

Katika maelezo yake, Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika kwa jina la Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku wala vipande vya kanga ambavyo mama amedai walimzikia mwanae miaka 4 iliyopita.

 

Katika zoezi hilo la kufukua kaburi yamepatikana mabaki ya fuvu la kichwa na mifupa ambapo jeshi la polisi limekabidhi sampuli hizo kwa Mkemia Mkuu wa serikali ili kupata vipimo vya vinasaba ili kujua undani wa tukio hilo.

 

Kamanda wa Polisi mkoani Geita Henry Mwaibambe amewaomba madaktari bingwa Hospitali za Muhimbili, Bugando na KCMC kumsaidia mtoto huyo matibabu ili aweze kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Leave A Reply