MTOTO ALIYENUSURIKA KUUAWA NJOMBE AFARIKI DUNIA – VIDEO

Mtoto Meshack Myonga (4)mkazi wa mji mwema Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo amefariki dunia juzi Jumamosi, Februari 9, 2019 akiwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya alipokuwa akiendelea na matibabu.

 

Mtoto huyo aliokotwa barabarani jirani na porini akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa koromeo Desemba 23 mwaka Jana majira ya saa 4 asubuhi mtaa wa mji mwema.

Toa comment