The House of Favourite Newspapers

MTOTO APATA SHAVU KAMPUNI YA AFYA YA KINYWA NA MENO

Afisa Habari JH, James Camilious (kulia) akieleza lengo la mkutano huo.

Kampuni ya JH ambao ni mawakala wa kusambaza dawa mpya ya meno iitwayo Lecan pamoja na visafishio vya meno juzi Jumamosi imeingia mkataba wa mwaka mmoja na balozi wake mpya mtoto Raniah Mohammed. Mkataba huo umesainiwa na wazazi wa mtoto huyo pamoja na maofisa JH Enterprises LTD.

Mwanasheria wa JH Mathew Kabunga (kulia) akiwaangalia wazazi wa Raniah, Mohammed Yahya ambaye ni baba yake na mama yake aitwae Shillah wanavyosaini mkataba huo.

Kampuni hiyo ambayo imeleta nchini huduma ya dawa za meno zenye ubora wa hali ya juu na kuweza kuondoa rangi mbaya ya meno inayotokana na uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe na vitu vingine vinavyoharibu meno.

Brand Meneja wa Kampuni hiyo, Husna Said (kushoto) na pamoja na Raniah na wazazi wake wakiwa na nyuso za tabasamu baada ya kumaliza zoezi la kusainishana mkataba huo.

Brand Meneja wa Kampuni hiyo, Husna Said akizungumza na wanahabari Bagamoyo, Pwani, alisema dawa hizo zitamaliza tatizo la meno na maradhi ya kinywa hapa nchini ambalo limeonekana kuwaathiri wengi.

Sehemu ya Bango la Kampuni hiyo.

Husna amesema hivi karibuni kampuni hiyo kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa meno kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kutumia kliniki yao ya Oral care watazunguuka nchi nzima kuitangaza na kuwasaidia wenye matatizo ya kinywa na meno.

HABARI NA RICHARD BUKOS GPL.

Comments are closed.