The House of Favourite Newspapers

BELLE 9 AANGUA KILIO BAADA YA KUONA JENEZA LA MASOGANGE

MSANII wa Bongo Fleva Abernego Damian ‘Belle 9’ ameshindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio mara baada ya kuliona jeneza lenye mwili wa msanii mwenzake, Agnes Gerald ‘Masogange’ ulipowasili nyumbani kwao, Utengule, Mbalizi mkoani Mbeya.

Baada ya kuona hali hiyo ya Belle 9, msanii wa Bongo Movie, Daudi Michael ‘Duma’ alisogea karibu na kujaribu kumtuliza Belle 9 na kumsihi asilie.

Belle 9 ndiye alimtambulisha Masogange kwenye tasnia ya sanaa katika wimbo wake uliokuwa gumuzo mwaka 2011 uitwao ‘Masogange’ ambapo Agnes ndiye alikuwa video Queen kwenye wimbo huo.

Pia wimbo huo wa Belle 9 ndiyo uliompa jina la Masogange ambalo amekuwa akitamba nalo hadi kufikwa umauti.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngomakilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao kuzikwa.

Mwili wa marehemu umewasili kijijini hapo mapema leo baada ya jana kuagwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

PICHA NA HILALLY DAUDI | GLOBAL TV ONLINE, UTENGULE, MBALIZI, MBEYA

Comments are closed.