The House of Favourite Newspapers

Mtoto: Baba Alimuua Mama Nikishuhudia

MONTGOMERY COUNTY, Texas

MTOTO wa miaka 11, amewaambia polisi tukio zima juu ya baba yake kumchoma kisu mama yake na kumuua.

Tukio hilo la kushtua lilitokea jana jioni Jijini Montgomery, Texas nchini Marekani ambapo mara baada ya mtoto huyo kumshuhudia baba yake, Medger Blake, 41 akimchoma kisu mama yake, Rose Blake, 38 aliwapigia polisi simu ambapo haraka sana wakafika eneo la tukio ambapo walimkuta mtoto huyo akiwa sebuleni huku ametapakaa damu.Kwa taarifa kutoka kituo cha polisi hapo Montgomery County zinasema kwamba hakukuwa na taarifa za ugomvi au viashiria vyovyote ambavyo vingewatia hofu kwa kuhisi kungekuwa na mauaji yatakayotokea.

“Mtoto alishuhudia baba akimchoma kisu mama yake na kututaarifu. Ni tukio lenye kuhuzunisha na tuliweza kufika eneo la tukio haraka sana,” alisema Kepteni Bryan Carlisle.

Polisi baada ya kufika eneo la tukio

Polisi walipofika nyumbani hapo, walimkosa Blake lakini baada ya dakika kadhaa wakamuona akiwafuata huku akiwa na kisu kilichokuwa na damu hali iliyowafanya polisi hao kumpiga risasi kama njia mojawapo ya kujihami.

Majirani kutoka katika nyumba iliyotokea tukio hilo walilizungumzia tukio hilo kwamba iliwashangaza kwani hapo kabla hakukuwa na dalili za ugomvi zaidi ya kumuona Blake akicheza na mtoto wake huku wakionekana kuwa na furaha.

“Hakuna aliyehisi kama kitu hiki kingetokea kwani mara kwa mara walikuwa wakicheza kwa furaha kiasi kwamba walihisi hakukuwa na tatizo lolote lile,” alisema jirani mmoja.

Comments are closed.