The House of Favourite Newspapers

Mtoto Ramadhani Shaibu Anatumia Mikono Kwenda chooni, Mama Yake Aomba Kusadiwa – Video

0

Mtoto Ramadhani Shaibu (14) mkazi wa Mbagala Kokoto yuko kwenye athari mbaya ya kupata magonjwa ya kuambukiza baada ya kutumia mikono kwenda chooni na kukaa kwenye choo cha chini kutokana na tatizo la ulemavu alilonalo ambapo mama yake hana uwezo wa kumtengenezea choo maalum kwaajili yake.

Akizungumza kwa uchungu sana mama wa mtoto huyo, Aisha Joseph, amesema kuwa mtoto wake huyo kila mara anapata maambukizi ya magonjwa ya njia ya mkojo, maana anakalia choo ambacho kinatumiwa na watu wengi na pia kutumia mikono kwenda chooni ambapo, hata akitoka hana sabuni maalum ya kusafisha mikono yake.

Kama umeguswa na habari hii mchangia mama huyo chochote kupitia namba yake ya mkononi O684940629 (Aisha Bakari) na Whatsaap waweza kuwasiliana nami kwa njia 0713612533 kwa maelezo zaidi.

Leave A Reply