The House of Favourite Newspapers

Watoto wa Bilionea Msuya Wamlilia JPM, Kupata Mali za Baba Yao – Video

WATOTO watatu wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi, mwaka 2013, wamemuomba Rais John Magufuli, kuwasaidia kuokoa mali za baba yao, ambazo wanahofu ya kunyang’anywa na ndugu wa baba yao.

 

Watoto hao amedai kuwa kwa sasa wamekosa mahali pa kuishi, licha ya baba yao kuacha mali nyingi tena za mabilioni ya pesa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, mtoto mkubwa wa Erasto, Kelvin Msuya alisema tangu baba yao, auawe  mwaka 2013 na baadaye mama yao mzazi, Miriam Steven Mrita, kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha shangazi yao, Annette Msuya, maisha yao yamekuwa ya tabu.

TAZAMA HAPA

Comments are closed.