The House of Favourite Newspapers

Menina Asimulia Kuhusu Video Yake ya Ngono – Video

HATIMAYE muigizaji, MC na mwanamuziki, Menina Abdulkharim, amefika katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuitikia wito wa baraza hilo lililomtaka kufika ofisini hapo kutoa maelezo juu ya video yake ya ngono inayosambaa mitandaoni.

 

BASATA kupitia Katibu Mtendaji wake, Godfrey Mngereza limetoa taarifa hiyo baada ya kikao na msanii huyo;

 

“Mara kadhaa BASATA kupitia utaratibu wake wa kutoa Elimu kwa wasanii na Umma wamekuwa wakiwaelekeza wasanii wote kote nchini kufanya kazi zao za Sanaa kwa kuzingatika maadili mema kwa jamii, pamoja na kufuata taratibu za kujisajili, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya wasanii wamekuwa hawazingatii maelekezo hayo na hivyo kujikuta wanavunja sheria za nchi.

“Kupitia mahojiano kati ya Msanii na BASATA kwa pamoja wamesikiliza maelezo ya Msanii Menina Abdulkarim na nini kilichojitokeza katika sakata zima la kusambaa kwa video na picha zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii.

“Kwa kuwa suala la kusambaa video na picha za utupu za Msanii Menina katika mitandao ya kijamii lipo mikononi mwa mamlaka nyingine, BASATA imeamua kuyafanyia kazi maelezo yake,” limesema BASATA.

MENINA ASIMULIA

Comments are closed.