The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Gaddafi Aruhusiwa Kuwania Urais

0

Mahakama ya nchini Libya imeamua kwamba Mtoto wa Gaddafi, Seif al Islam anaruhusiwa kugombea kiti cha Urais nchini humo na hivyo kuubatilisha uamuzi wa hapo awali uliopitishwa na Tum ya Uchaguzi ya Libya.

Tume hiyo ya Uchaguzi ilisema kuwa Seif al-Islam Gaddafi hakukidhi vigezo kugombea Urais, Seif al-Islam alikata rufani dhidi ya uamuzi wa Tume hiyo.

Mahakama ya jimbo la Sabha imeamua kumpitisha Mtoto huyo wa Gaddafi, hatua inayompa nafasi ya kusimama katika uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Desemba 24, mwaka huu.

Leave A Reply