The House of Favourite Newspapers

MTOTO WA KIGWANGALLA AZIKWA NZEGA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan aliongoza shughuli za mazishi ya Zulqarinain mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla yaliyofanyika jana Ijumaa Februari 22, 2019 majira ya saa 10 jioni katika Kijiji cha Puge, Nzega mkoani Tabora.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya Mawaziri, Manaibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Wabunge pamoja na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, watumishi wa TAMISEMI.

Marehemu Zul alifikwa na umauti juzi Alhamisi, Februari 21, 2019 majira ya saa 4 asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akitibiwa matatizo ya moyo.

MATESO Ya Mtoto HAMIS, Anayemlea Asimulia ya Kukutoa MACHOZI!

Comments are closed.