Mtoto wa Tanasha ampa wazimu Esma

MTOTO wa mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Natasha Donna Oketch amemtia wazimu dada wa mwanamuziki huyo, Esma Khan kutokana na kumsubiri kwa hamu. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Esma alisema, siku zote raha ya wifi ni mtoto ndiyo maana muda wote alimuomba Mungu afanye wepesi kwa wifi yake Tanasha ambaye alijifungua salama juzi (Jumatano).

“Kwa kweli huwezi kuamini, yaani huyu mtoto wa Tanasha amenipa wazimu, bora tu amekuja nitulie maana si unajua raha ya wifi mtoto! Basi hapa moyo una furaha tu kumpakata mwanangu,” alisema Esma.

stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment