The House of Favourite Newspapers

Bongo Fleva; MTV Base Africa Yawataja 5 Hawa Kama Wasanii Wa Kuwaangalia Zaidi Kwa Mwaka 2017.

Wasanii wa Bongo Fleva wanazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye nchi mbalimbali za Kiafrika.

Nimekutana na stori kwenye mtandao wa MTV Base kituo kikubwa cha burudani South Africa na Africa kwa ujumla ambapo wametoa list ya “wasanii wa kuwaangalia kwa (Ones To Watch 2017)” kwa mwaka huu wa 2017. Kwenye kuperuz listi hiyo ya wasanii 54 nikatutana na majina ya wasanii watano kutoka Tanzania ambao kwa mujibu wa MTV Base ni wasanii wanaoamini kuwa na uwezo wa kuleta kitu tofauti mwaka huu wa 2017. Wasanii hao ni; Ben Pol, Billnas, Ray Vanny, Harmonize na Ruby.

MTV Base inalenga kuwapa support wasanii hawa kadri wawezavyo ikiwemo kuwasaidia kujenga na kutangaza profile zao online, ku-support video zao pamoja na kuwashirikisha kwenye event zote kubwa na ndogo za MTV Base.

>> “Ones To Watch ni list ya wasanii inayotolewa kila mwaka, pia ni list ya wasanii tunaotegemea vitu vikubwa kutoka kwao kwa mwaka husika. Inafurahisha na kutia moyo sana kuona ni jinsi gani ambavyo wasanii kwenye list ya mwaka 2016 wamepiga hatua kubwa kwenye muziki na jinsi gani ambavyo support yetu imesaidia kwa namna moja ama nyingine kujenga profile na brand zao pote ndani na nje ya nchi.” << – Monde Twala, Vice President wa BET, Youth & Music na VIMN Africa.

Listi ya “Ones to Watch” hutolewa kila mwaka kama sehemu ya kutaka kuchunguza zaidi uwezo wa msanii kwenye vitu mbalimbali ikiwemo; potential yake kimuziki kwa sasa na badaae, mapato anayoyapata kutokana na idadi ya shows anazofanya, yupo active kwa kiasi gani kuachia kazi mpya, umaarfu wake ndani na nje ya nchi, radio na video airplay, muonekano na style yake, na vitu vingine vingi ambazo sio rahisi kuvitambua kwa jicho la kawaida. – MTV Base.

Unaweza kuicheki listi nzima ya wasanii kwa kubonyeza hapa.

Comments are closed.