The House of Favourite Newspapers

Linex Kusherekea Siku Yake ya Kuzaliwa kwa Staili Hii

Sunday Mangu ‘Linex’,

MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva anayefanya poa kwa sasa na ngoma yake ya Kiherehere, Sunday Mangu ‘Linex’, anatarajia kufanya sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa leo pamoja na watoto yatima.  

Linex amefunguka kuwa kila ifikapo tarehe 14 mwezi Februari amekuwa akifanya mambo mbalimbali kama kuwatembea watoto yatima, wagonjwa hospitalini ikiwa ni kama ishara ya kuhidhimisha siku yake hii ya kuzaliwa.

Sunday Mangu ‘Linex’,

“Mimi ni mtu wa Mungu, naijua Biblia vizuri hivyo muda wangu mwingi huwa namuuliza Mungu nifanye nini, leo imenijia tu akilini kuwa nifanye sherehe hii na watoto yatima. Naamini ni Mungu ndio amepanga mwaka huu nisherehekee kwa namna hiyo,” alisema Linex.

Msanii huyo amepanga kutembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.