The House of Favourite Newspapers

Mugabe Ahutubia Taifa, Akataa Kujiuzulu

0
Rais Mugabe akihitubia kwenye televisheni jana.

RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe amekataa shinikizo la kujiuzulu akisisitiza kwamba atauongoza mkutano mkuu wa chama tawala ambao utafanyika mwezi ujao.

 

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 alikuwa anategemewa kujiuzulu katika hotuba yake jana (Jumapili) kwa taifa, ikiwa ni siku tano baada ya jeshi kuchukua uongozi wa nchi hiyo na kumweka Mugabe chini ya ulinzi nyumbani kwake.

 

Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye televisheni kutoka ofisi yake ya Ikulu jana, Mugabe alikubali kukosolewa kunakofanywa dhidi yake  lakini alitaka nchi “irejee katika hali yake ya kawaida”.  Aliyasema hayo bila kutoa kauli ya aina yoyote kuhusu nafasi yake ya urais.

 

“Pamoja na yote yaliyofanywa na jeshi, mimi, nikiwa jemadari mkuu wa majeshi, nakubaliana na mawazo yao,” alisema Mugabe akiwa amekaa pamoja na viongozi wa jeshi.

 

“Lazima tujifunze kusamehe na kutatua matatizo ya kweli au yenye kuwazika, katika moyo wa kirafiki kama watu wa Zimbabwe,” aliongeza.

 

Hayo yamenyika katika wiki iliyojaa matukio mbalimbali ambapo jeshi lilichukua uongozi wa nchi na mitaa kufurika maelfu ya watu  kuliunga mkono jeshi na kumtaka Mugabe aondoke madarakani.

 

Jana chama tawala cha ZANU-PF kilitangaza kumvua uenyekiti wake na kumpa hadi leo mchana ajiuzulu nafasi ya urais la sivyo akabiliwe na mashitaka.

NA WALUSANGA NDAKI/GPL

Leave A Reply