The House of Favourite Newspapers

Mume aMuua Mke kwa Panga Akimtuhumu Kumsaliti

0

MWANAUME anayejulikana kwa jina la Heneriko John (53) mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, amedaiwa kumuuwa mke wake Regina Jiyenze (45) kwa kumkata mapanga kichwani na mabegani, kisha kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi.

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 5, saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Mbulu Kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

 

Kyando amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yao, kitendo ambacho kilimfanya mtuhumiwa kujichukulia sheria mkononi na kumkata mapanga na kusababisha mauaji.

 

“Katika eneo la tukio tumeokota panga lenye damu likiwa umbali wa mita 20 kutoka katika eneo la tukio lilipotendeka, mtuhumiwa tunamshikilia mara baada ya kujisalimisha mwenyewe, na tutamfikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” amesema Kyando.

 

“Mtuhumiwa alitumia mbinu ya kumvizia mke wake na kumkata mapanga wakati akiwa nyumbani kwa balozi Manungu Bundala, alipofika kwa ajili ya kushitaki kutishiwa kuuawa na mume wake, ndipo alipokatwa mapanga sehemu za kichwani na mabegani na kufariki dunia,” amesema.

 

Aidha, kamanda alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kisa wivu wa mapenzi, kwani kitendo hicho hakifai na kinaonekana kimekuwa sugu.

 

Ametoa ushauri kwa wapenzi au wanandoa, kuwa wakiona mwenzake sio mwaminifu kwenye mahusiano ni bora waachane kuliko kuchukua hatua mbaya kama hiyo.

 

Leave A Reply