The House of Favourite Newspapers

Mume hachungwi kwa simu shoga!

0

wife-cheatingAsalam alaikum wapenzi wasomaji wa kona hii, Shangingi nimerudi tena, leo hii nimeamua kuliongelea suala hili la simu jamani, zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kuvunja ndoa zetu.

Kutokana na kuvunja ndoa nyingi, wapo ambao mpaka sasa hawapendi kabisa kumiliki simu kwani zimewaumiza sana.

Lakini wakati hali ikiwa hivyo, bado wapo ambao wako kwenye uhusiano lakini wamekuwa wakizitumia vibaya simu zao. Unakuta mume wa mtu lakini ana namba za wanawake kibao kwenye simu yake na akiwa mbali na mwenza wake, ni mwendo wa kuchati na kuongea nao mambo yao wanayoyajua, sasa sijui ili iweje wakati ashaitwa mume wa mtu.

Hivyohivyo kwa wanawake, wapo ambao wana wapenzi lakini mawasiliano na vijibwana vya nje yamekuwa yakiendelea kama kawaida, pale wanapokuwa mbali na upeo wa macho ya wapenzi wao. Hii ni hatari sana.
Hatari zaidi inakuja pale ambapo unagundua kuwa hakuna mwanaume au mwanamke anayeweza kudiriki kumuachia mwenza wake simu yake kwa siku nzima.

Achilia mbali kumuachia, hata kuigusa tu ugomvi mkubwa unaweza kuibuka. Kwa nini? Kwa sababu ni watu wachache sana ambao simu zao hazina madhambi.

Sasa basi kwa sababu kila mmoja hawezi kugusa simu ya mwenzake basi wewe mwenye wivu wa kupindukia nakusihi sana usiiguse simu ya mwenza wako kwani ukiigusa ndiyo chanzo cha ugomvi.

Lakini nipongeze tu watu wanaopenda kugusa simu za wenzao, kuzipekua huwa na tabia ya kuchepuka, sasa anahisi na mwenzake anachepuka ndiyo maana hutokea mambo makubwa mpaka kufikia kuvunja ndoa.
Hivi kama unaweza kumvumilia mumeo, akashinda kazini au mkeo ni kwa nini usiivumilie hata simu yake, kwani zamani wakati simu hazijatoka watu walikuwa hawachepuki? Jibu unalo..

Haya je, hakuna watoto waliozaliwa zamani na wamama kuwapa wababa watoto wasio wao, sasa kwa nini suala la simu livunje ndoa yako rafiki yangu, wewe jiamini mpaka umeingia naye kwenye ndoa, jua wewe ndiyo kila kitu.

Fanya kama vile huoni uone kama ndoa yako itatetereka, unaweza kushinda na simu ya mwenza wako tangu asubuhi na usibaini lolote, je ndiyo kwamba ni mtakatifu? Hapana anaweza kuwa anachepuka lakini si kwa kutumia simu.
Au anaweza kuwa anatumia simu lakini ameweka sharti kwa mchepuko mpaka saa flani usinipigie simu, akili kichwani kwako mume hachungwi kwa simu.

Leave A Reply