The House of Favourite Newspapers

Mume wa Zamaradi Afikishwa Kortini kwa Kutishia Kuua – Video

MUME wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi leo Jumatatu, Novemba 4, 2019, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na kosa la kumtishia kumuua kwa kutumia bastola, Dereva wa lori la mchanga Venance John.

 

Shaban amefikishwa mahakamani hapo akitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kesi yake kushindwa kusajiliwa mahakamani hapo.

 

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga mbele ya Hakimu Mfawidhi, Frank Moshi, ambapo inadaiwa tukio hilo amelitenda Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Mbezi Mabwepande.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Inadaiwa alikutwa na Pistol aina ya Berreta yenye namba za usajili 102969 ambapo kwa makusudi alimtishia Venance John huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, baada ya kusomewa shtaka lake amekana na upande wa mashitaka ukasema hauna pingamizi na dhamana.

 

Baada ya kueleza hayo, Hamisi ameachiwa kwa dhamana baada ya kukidhi vigezo vya kuwa na Wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho vya Taifa na wamesaini Bondi ya Sh.Mil 2 kwa kila mmoja na kesi hiyo imeahirishwa hadi November 13, mwaka huu.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

 

Katika video iliyosambaa mitandao, dereva wa gari kubwa (Venance John) alianza kusikika akimwambia mume huyo wa Zamaradi kuwa; “umesema unatoa bunduki itoe hiyo bunduki.”

 

Wakati mzozo huo ukiendelea, dereva wa gari dogo ambaye ndiye mume huyo wa Zamaradi, aliyekuwa amevaa shati jeupe, alielekea katika gari lake na kutoka na bastola.

 

 

Pamoja na kutoka na bastola, dereva wa gari kubwa hakuonyesha kutishika na kitendo hicho na kumwambia kuwa kama anataka kumshambulia kwa bastola haogopi kwa sababu alizaliwa ni lazima atakufa.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

“Mimi kufa nitakufa na wewe utakufa, huna lolote, nakwambia kweli huna lolote, toa hiyo bunduki, mwache aniue,” alisikika akisema dereva wa gari kubwa.

Licha ya Shaban kumwamuru akae chini huku akitoa maneno makali, bado dereva huyo alikataa huku akisisitia kuwa kama anataka amuue. Pia Shaban alionekana akimwelekezea kichwani mwenzake bastola hiyo na kumweleza kuwa atampasua.

Comments are closed.