The House of Favourite Newspapers

Mume Wangu Anaishi Mara ya Pili-16

0

Ilipoishia wiki iliyopita:

“Mama Kisu, yule mwanaume ni pacha wa baba Kisu?”
Endelea mwenyewe sasa:
“Kwa nini?” nilimuuliza yule mwanamke.
“Wamefanana kila kitu. Yaani kwanza nilishtuka, nikasema huyu baba Kisu si amezikwa juzijuzi tu, imekuaje tena? Nini kimetokea!”

Moyoni nilishangaa sana, mimi ninavyomuona Tiaki na marehemu mume wangu hawafanani hata kwa kulazimisha, baba Kisu alikuwa mng’avu sana, Tiaki mweusi tii. Yaani hawakufanana hata kidogo.
“Au hata Kisu anamwona hivyo ndiyo maana akasema shikamoo baba?” nilijiuliza.
“Hapana, mbona siyo mapacha. Kwani wanafanana?” niliuliza.
“Jamani mama Kisu, lakini ni ndugu?”
“Wala.”

“Mh! Basi kuna jambo,” alisema yule mwanamke.
Niliondoka, kufika nyumbani, msichana wa kazi akaniambia kuna mwanaume hamjui, ameleta barua, nikaipokea na kukaa kuisoma. Iliandikwa kwa ufupi sana…
“Mama Kisu, pole kwa yote. Ukweli kifo changu hakikuwa cha kawaida. Nakushukuru kwa kunitambua. Nakutakia maisha mema, narudi niliko. Mimi baba Kisu.”

Nilianguka, nikapoteza fahamu. Nilikuja kuzinduka nikiwa hospitali na baadhi ya majirani ambao niliwasimulia kisa chote. Nao wakasema:
“Mh! Pole sana mama Kisu. Kwa hiyo kumbe mumeo alikuwa akiishi mara ya pili.”
MWISHO.

Leave A Reply