The House of Favourite Newspapers

Musonye Aigwaya Yanga, Aifungia Gormahia

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye.

CECAFA imegwaya kuiadhibu Yanga na ikaishia kuitupia mpira TFF, huku ikiwafungia Gormahia miaka miwili kushiriki mashindano ya Kagame baada ya wachezaji wake kugomea medali za mshindi wa tatu juzi Ijumaa.

 

Wachezaji hao waligoma kama njia ya kushinikiza uongozi wao uwalipe posho mshahara wa mwezi mmoja wanaodai. Habari zinasema kwamba wachezaji hao walicheza mechi dhidi ya JKU na kushinda mabao 2-0 na waliamua kutogomea mechi ili wapate mgawo wao wagawane.

 

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema; “Kocha wa Gor Mahia naye alikuwa akitoa maneno ya matusi kwa marefa hilo tumeliona kwenye ripoti hivyo tunataka kuonesha kwamba tuna misimamo na kwa kila timu itakayofanya makosa tutaiadhibu.”

 

“Kuna timu ambayo haikushiriki ikiwa na imani kwamba tutashindwa kufanya vizuri hilo litakuwa chini ya TFF na kama tukiandaa mwakani wakajitoa hatuna mashaka tutaendelea kufanya mashindano bila kuangalia ukubwa wa timu,” alisema Musonye akionekana kuitupia madongo Yanga.

 

Habari zinasema kwamba Musonye na kamati yake wameigwaya Yanga kwavile kuna uwezekano mkubwa mashindano yajayo yakarudi Dar es Salaam kutokana na hali ya uchumi ya nchi washirika.

 

Azam juzi ilitwaa ubingwa wa Kagame baada ya kuifunga Simba kwenye fainali. Ilijipatia Sh68milioni ambazo watakabidhiwa kesho Jumatatu huku Simba ikiambulia Sh45milioni.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA NA ISAYA MBENA

Comments are closed.