The House of Favourite Newspapers

Mussa Sima Apania Kuigeuza Singida Kuwa Jiji

0

Mgombea Ubunge jimbo la Singida mjini kupitia CCM, Mussa Sima amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kumalizia kutatua changamoto zilizopo katika jimbo hilo na kuhakikisha mji huo unapanda hadhi na kuwa jiji.

 

Sima ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa jimbo hilo na kuwaelezea mambo yaliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano.

” Ndugu jukumu mlilotupatia katika kipindi cha miaka mitano, mji huu umebadilika. Mji huu sio ule. Na leo tunazungumza juu ya maendeleo kwa sababu lengo langu ni kuufanya mji huu kuwa jiji, tuna jiji jirani la Dodoma lakini halina miundombinu kama tuliyonayo sisi. Ukienda kuangalia na kuja hapa Singida utapata majibu,” alisema.

Aidha, aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa kura za kutosha ili kumalizia changamoto zilizosalia sambamba na kumchagua mgombea urais Dk. John Magufuli pamoja na madiwani 18 wa jimbo hilo.

 

” Pamoja na mafanikio hayo tunajua kuna changamoto chache ambazo ni barabara na mitaro kwa sababu hii kata ya Utemini ipo chini, mvua ikinyesha maji yote yanakuja huku na tusipotengeneza miundombinu maji yanatwama. Hii ndio kazi mnayotutuma… sisi tunajua tatizo hili hao wengine hawajui kama ninyi mna matatizo haya na wataenda kumuomba nani fedha ya kutatua tatizo la mitaro?

“Kuna bajeti ya dharura tuliyoitengeneza, leo hii fedha zikiingia tunajua vipaumbele ni vipi kwa sababu kazi yetu ni ndogo tu. Fedha ikiingia ni kupanga fedha hizi zielekezwe kwenye kata ya Utemini ambayo ni kipaumbele chetu.

 

” Haya ninawaeleza kwa sababu sisi ni wafuasi wake (Magufuli) ambao ametuamini. Wewe fikiria kati ya wabunge 400 ananiteua mimi kuwa Naibu waziri kwa niaba yenu, hiyo maana yake mimi ni mtumishi mwaminifu.

” Sasa anawezaje kusimama mtu na kunikosoa mimi maana yake anamkosoa Rais na anamkosoa Mungu vilevile… mtu anayemkosoa Mwenyezi Mungu huyo si shetani. Sasa utamuamini vipi shetani?

 

Aidha, aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa kura za kishindo Oktoba 28 ili kuhakikisha mji huo unaendelea kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Na Mwandishi wetu

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave A Reply