The House of Favourite Newspapers

Muuguzi Ajinyonga Hadi Kufa Kisa Madeni

0

MUUGUZI wa Hospitali ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, David Mtaita (30) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ikiwa ni baada ya kujichoma sindano ya kutuliza maumivu.

 

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 29, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa katika uchunguzi wa awali wamebaini muuguzi huyo alijinyonga juzi saa 12 jioni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni.

 

Amesema kabla ya kujinyonga alijichoma sindano ya kutuliza maumivu kwa kuwa ilikutwa pembeni ya mwili wake.

 

“Alifanya kitendo hicho katika nyumba aliyokuwa anaishi eneo la Singisi wilayani Arumeru,” amesema na kubainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Leave A Reply