The House of Favourite Newspapers

Muvi ya Black Panther yatisha Tuzo za MTV 2018

TUKIRUKA majuu kiaina, juzi usiku (Jumatatu), kwenye ugawaji wa Tuzo za MTV Movie & TV, ulikuwa ni usiku mkubwa kwa mara nyingine kwa Kampuni ya Marvel, pamoja na timu nzima iliyofanikisha kutoka kwa Muvi ya Black Panther, baada ya kutwaa Tuzo ya Filamu Bora (Best Movie), huku waigizaji wake wengine pia wakijizolea tuzo kibao.

Waliyojizolea tuzo hizo ni Chadwick Boseman ‘T’Challa’, aliyebeba tuzo mbili na hasimu wake mkubwa kwenye muvi hiyo Michael B. Jordan ‘Erik Killmonger’, aliyevuna tuzo moja. Cheki washindi wote kwa jumla;

FILAMU BORA (BEST MOVIE)

Zilizoshindanishwa; Avengers: Infinity War iliyoandaliwa na Kampuni ya Walt Disney Studios Motion Pictures, Black Panther (Marvel Comics), Girls Trip (Universal Pictures), IT (New Line Cinema), Wonder Woman (Warner Bros. Pictures).

Iliyoshinda; Black Panther.

MCHEZO BORA (BEST SHOW)

Zilizoshindanishwa; 13 Reasons Why iliyokuwa inaonyeshwa na Netflix, Game of Thrones (HBO), Grown-ish (Freeform), Riverdale (The CW).

Iliyoshinda; Stranger Things.

***

 

MCHEZAJI BORA KWENYE MUVI (BEST PERFOMANCE IN A MOVIE)

Walioshindanishwa; Timothée Chalamet aliyecheza kwenye Filamu ya Call Me by Your Name, Ansel Elgort (Baby Driver), Chadwick Boseman (Black Panther), Daisy Ridley (Star Wars: The Last Jedi na Saoirse Ronan (Lady Bird).

Mshindi; Chadwick Boseman.

***

MCHEZAJI BORA KWENYE MCHEZO

Walioshindanishwa; Darren Criss, aliyeshiriki kwenye Mchezo wa The Assassination of Gianni Versace: American Crime Story, Katherine Langford (13 Reasons Why, Issa Rae – Insecure), Maisie Williams (Game of Thrones) na Millie Bobby Brown (Stranger Things).

Aliyeshinda; Millie Bobby Brown.

***

 

SHUJAA BORA (BEST HERO)

Walioshi-ndanishwa; Emilia Clarke aliyecheza kama Daenerys Targaryen – Game of Thrones, Gal Gadot (Diana Prince/Wonder Woman), Grant Gustin (Barry Allen/ The Flash), Daisy Ridley (Rey) – Star Wars: The Last Jedi na Chadwick Boseman (T’Challa/Black Panther) – Black Panther.

Mshindi; T’Challa.

***

MCHEKE-SHAJI BORA

Walioshin-danishwa; Jack Black aliyecheza kwenye Jumanji: Welcome to the Jungle,Tiffany Haddish (Girls Trip), Dan Levy (Schitt’s Creek), Kate McKinnon (Saturday Night Live) na Amy Schumer ( I Feel Pretty).

Mshindi; Tiffany Haddish.

***

PAMBANO BORA (BEST FIGHT)

Walioshind-anishwa; Muvi ya Atomic Blonde. Charlize Theron (Lorraine) vs. Daniel Hargrave (Sniper) na Greg Rementer (Spotter). Avengers: Infinity War – Scarlett Johansson (Natasha Romanoff/ Black Widow), Danai Gurira (Okoye), Elizabeth Olsen (Wanda Maximoff/ Scarlet Witch) vs. Carrie Coon (Proxima Midnight). Black Panther – Chadwick Boseman (Black Panther) vs. Winston Duke (M’Baku). Thor: Ragnarok – Mark Ruffalo (Hulk) vs. Chris Hemsworth (Thor).

Mshindi; Wonder Woman – Gal Gadot (Wonder Woman) vs. German Soldiers

***

TAMTHILIA BORA YA KWELI (BEST REALITY SERIES)

Zilizoshindanishwa; The Kardashians, Love & Hip Hop, Real Housewives, RuPaul’s Drag Race, Vanderpump Rules.

Mshindi; The Kardashians.

STORI:BONIPHACE NGUMIJE.

Comments are closed.