The House of Favourite Newspapers

Mvua yaitibulia Simba Dar

 

WAKATI Simba ikielekea hatua zake za mwisho kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara jana ilishindwa kufanya mazoezi kama ilivyojipanga kutokana na mvua na foleni ambazo ziliwakwamisha wachezaji.

 

Simba ilitua Dar siku ya Jumatatu ikitokea jijini Mbeya ambako ilicheza dhidi ya Prisons na Mbeya City. Na leo Jumatano itakuwa ikivaana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Uhuru jijini hapa. Simba ilitakiwa kufanya mazoezi yake jana Jumanne asubuhi katika Uwanja wa Uhuru lakini ilishindikana kutokana na mvua na wachezaji kushindwa kukutana kwa wakati kutokana na foleni.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema; “Mazoezi tulitakiwa kufanya leo(Jumanne) asubuhi pale katika Uwanja wa Uhuru lakini hali ya hewa na mvua imetibua na wachezaji wengi wamekwama kwenye mafoleni.”

 

“Na imekuwa ngumu sababu Jumatatu tulipofika hapa wachezaji walienda majumbani mwao lakini kama wangekuwa kambini ingekuwa ni rahisi kwetu kutafuta popote tuweze kupasha kwa ajili ya mchezo wa kesho. “ Lakini kama hali itaendelea hivi ya mvua basi huenda tusifanye kabisa au tukipata nafasi tutafanya popote pale ilikujiweka sawa sababu mchezo ambao tunaenda kucheza siyo rahisi lazima tujipange,”alisema Patrick.

 

Kwa upande wa Coastal Union, kocha Juma Mgunda alisema : “Mvua imetuvuruga ilikuwa tuende pale Uhuru kufanya mazoezi ya mwisho lakini tutapasha tu kidogo sababu jana Jumatatu tulipata nafasi ya kufanya mazoezi. “Tunaenda kukutana na timu kubwa yenye uwezo na wachezaji wazuri lakini upande wetu kama timu kumejipanga kuhakikisha tunapointi tatu muhimu.”

STORI NA MARTHA MBOMA

Comments are closed.