The House of Favourite Newspapers

Mwambusi Atangaza Kurejea Yanga

0

ALIYEKUWA Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema kwa sasa yupo fiti kurejea kikosini hapo baada ya kufanyiwa upasuaji wa jino.

Hivi karibuni, Mwambusi aliachia nafasi ya kukinoa kikosi cha Yanga baada ya kupata matatizo ya kiafya. Nafasi yake imechukuliwa na Nizar Khalfan.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwambusi alisema: “Nimefanyiwa upasuaji kwenye jino na tayari nina wiki mbili, naendelea vizuri, sisikii maumivu tena kama mwanzo.

 

“Naona kuna mabadiliko na nitarudi tena hospitali Jumatano ili kujua maendeleo zaidi, endapo nitakuwa sawa naweza kurejea Yanga.

 

“Wanamichezo waniombee nipone ili niweze kurejea katika majukumu yangu kama zamani.”

STORI: LEEN ESSAU, Dar es Salaam

SENZO APATA KIGUGUMIZI, ISHU ya KOCHA KAZE Kubaki YANGA – “SARE NYINGI IMELETA TATIZO”…

Leave A Reply