The House of Favourite Newspapers

Harmo: Kajala Akiniacha Naweza Kujiua

0
Kajala na Harmonize

UNAAMBIWAstaa anayefanya poa kwa sasa kunako Bongo Fleva, Rajab Abdul almaarufu Harmonize au Konde Boy, amenyoosha maelezo kwa mpenzi wake wa sasa, Kajala Masanja na kusema; “Kwa upendo anaonionesha, akiniacha naweza kujiua!

 

”Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kwamba, kapo ya Kajala na Harmonize kwa sasa ndiyo kapo inayotamaniwa zaidi na kupendwa na wengi ukilinganisha na kapo nyingine za mastaa Bongo.

 

Kwa mujibu wa Harmonize au Harmo, hakuzoea matunzo na mambo mazuri na mazito ambayo anayapata sasa hivi kutoka kwa Kajala ambaye ni staa wa Bongo Movies.

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kwamba, awali, kabla ya Harmo kuwa na Kajala, kuna huduma ya mambo mazito ambayo alikuwa hayapati, lakini kwa sasa anayapata na zaidi yake kutoka kwa Kajala.

 

Kwa mfano; kabla ya kuwa na Kajala, Harmo hakuonekana akishukuru kwa kupatiwa kifungua kinywa (breakfast) ya mchemsho wa samaki aina ya sato asubuhiasubuhi, lakini sasa anatupia tu vipande vya video akifurahia misosi mizuri kutoka kwa mwanamama huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula Paul.

 

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Kajala na Harmo, jamaa huyo hakuzoea staili hiyo ya maisha na zaidi sana alikuwa akiishi kigetogeto.“Jamaa alizoea kupiga pasi ndefu (kupitiliza muda wa kula au kula mara moja kwa siku) na mambo ya vyakula vya mtaani, lakini sasa hivi anakula kwa kufuata ratiba.

 

“Angalia ile video ya mchemsho wa samaki alioandaliwa na Harmonize, alikuwa anashukuru na kukiri kwamba sasa hivi ananenepa kiasi cha watu kumuita mbavu,” anasema mtu huyo wa ndani wa wawili hao na kuongeza;“Kajala amekuwa akimwambia asijali na atazoea maisha hayo na atarajie mengi yanakuja.

 

”Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA, Harmo au Jeshi ambaye ni Mkurugenzi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide anasema kuwa, ameingia mzimamzima kwa Kajala na anaamini ndiye alikuwa chaguo lake sahihi.Hata hivyo, Harmo anamtahadharisha Kajala kwamba kama ataleta mambo yasiyoelewa kwenye mapenzi yao hayo, basi ajue anatembea na damu ya moyo wake hivyo kuendelea kuishi itakuwa ni ngumu.Kwa mahojiano kamili na Harmo; funua kurasa za 10 na 11.

Stori:IMELDA MTEMA, Dar

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply