The House of Favourite Newspapers

Mwana FA Avunja Rekodi Mapokezi Muheza

0
Mgombea Ubunge Jimbo la Muheza, Hamis Mwinjuma alimaarufu Mwana FA, baada ya kupokea fomu za kuwania ubunge jimbo hilo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi, Nassib Mbaga.

MAPOKEZI ya mgombea ubunge Jimbo la Muheza (CCM), Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA,  jana amevunja rekodi ya umati wa mapokzi katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga huku akihaidi kupigania mahitaji ya wasanii pindi akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu.

…Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufika ofisi za CCM wilaya ya Muheza; kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Muheza, Mohamed Moyo

 

MwanaFA pia alishangazwa na mapokezi aliyopata kutoka kwa wananchi wa wilaya ya Muheza, hali ambayo ilimtoa machozi na kusimamisha huduma mjini Muheza kwa muda wa saa mbili  kuanzia muda wa saa 5:00 asubuhi hadi saa 7:00 kamili mchana.
 

…Akiwa na Mohamed Moyo wakitoka ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo.

Msafara wa kwenda kumpokea MwanaFA kutoka kijijini kwao Kwemhanya kata ya Mtindiro ulianza kuondoka Muheza mjini majira ya saa 4:30 asubuhi kuelekea katika kijiji cha Kibanda umbali wa kilometa saba kutoka Muheza Mjini.

Mapokezi yakindelea.

Majira ya saa 5:00 asubuhi MwanaFA aliwasili katika kijiji cha Kibanda katika barabara kuu ya Tanga-Segera ambapo alikuta umati mkubwa wa watu ukimsubiri wakiwa kwa miguu, magari na bodaboda, jambo ambalo lilimfanya ataharuki na kutoa machozi.
 

KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Muheza akizungumza wakati wa halfa hiyo.

Msafara ulianza kuelekea kuliekea hadi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM wilayani Muheza 11:43 akisindikizwa katika gari la wazi huku akiifuatuliza nyimbo zake ambapo alikwenda kusaini katika kitabu cha wageni baada ya hapo alitembea kwa miguu kwa maandamano kupitia barabara ya soko kuu la mbogamboga na matunda-Amtco -stendi kuu-hadi Bomani katika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Muheza.

Saa 6:17 Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Muheza Nasibu Mbaga alikabidhi fomu nne za NEC na kupewa maelekezo ya namna ya kuzijaza ambapo alikuwa ni mgombea wa saba huku akitanguliwa na wagombea wengine wa ubunge wa jimbo hilo kupitia vyama vya CUF, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, UDP, na AAFP.

Saa 6:19 alitia saini katika kitabu cha wageni cha NEC na kuondoka kuelekea tena katika ofisi za CCM Muheza ambapo alifika majira ya saa 6:45 ambapo aliongea na wananchi.

Saa 7:00 alimaliza kuongea na majira ya saa 7:31 alifanyiwa tambiko za kimila za kabila la Wabondei.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu za NEC alisema kuwa amesukumwa kuja kugombea jimbo la Muheza kutokana na kero mbili kuu ambazo kwa muda mrefu limekuwa ni tatizo sugu kwa wananchi wa Muheza ambazo ni changamoto ya maji na barabara ya Muheza- Amani yenye urefu wa kilometa 35 ambayo ipo katika kiwango cha changarawe ambapo katika kipindi cha mvua huwa haipitiki.

“Watu wote tunajua kuwa Muheza kuna tatizo la maji,kwa mara ya kwanza nilikutana na mama mmoja akinionyesha kichwa chake kimonyonyoka nywele akaniambia ni kwa sababu ya kubeba maji,na pili wenzetu wa Amani wanapata tabu sana kwenye kipindi cha mvua barabara haipitiki,” alisema.

 

Kuhusu maslahi ya wasanii amesema “nitahakikisha ninatetea mahitaji ya wasanii kwa jumla nikiwa bungeni kutokana nitakuwa mmoja kati ya watunga sheria,hivyo wasanii sitawaangusha.”

 

Saa 8:00 aliondoka Muheza ambapo aliongozana na bondia wa ngumi za kulipwa, Hassan Mwakinyo, ambaye alipokelewa katika mji wa Pongwe akitokea Dar es Salaam baada ya pambano lake la ngumi la kimataifa hivi karibuni jijini Dar.

Leave A Reply