The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Akutwa Ameuawa Chumba cha Kupanga

0

MWANAFUNZI mmoja wa Chuo cha KMTC mwenye umri wa miaka 23 amekutwa amefariki kwenywe nyumba yake aliyokuwa amepanga huko Oriang Estate, Homabay nchini Kenya huku akiwa na majeraha makubwa.

 

Hata hivyo polisi baada ya kupata taarifa hiyo wamefika eneo la tukio na kushangazwa kwa kile walichokiona kwa binti huyo, hivyo wameanza kufanya uchunguzi wao ili kuweza kupata chanzo.

 

Emily Chepkemoi ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha mafunzo ya tiba nchini Kenya ilisemekana amepotea ghafla wala simu yake haipatikani.

 

Hata hivyo baada ya kuona hivyo waliamua kwenda nyumbani kwake ili wakamusalimie lakini cha ajabu ni kwamba walikuta mwili wa mwanafunzi huyo ukiwa tayari umeshajeruhiwa na kupoteza maisha.

 

Majirani wa mtaa huo pia walishangaa kwani wanadai kuwa toka ameingia ndani mwake Ijumaa hawakumwona akitoka nje, lakini badala yake wakaanza kusikia harufu mbaya kutoka chumbani kwake.

Hata hivyo Dancun Oketch, Mkuu wa Msaidizi wa eneo hilo alisema kuwa mwili wa Chepkemoi ulikuwa na majeraha kadhaa ya kuchomwa na kwamba kifo chake kinasadikika kuwa ni matokeo ya kuchepuka.

 

Polisi wapo kwenye uchunguzi na kuhakikisha wanampata ambaye alikuwa mpenzi halisi wa binti huyo pamoja na yule aliyekuwa anachepuka naye ili waweze kujua nani ambaye amehusika katika mauaji hayo.

 

Hata hivyo marafiki zake walilia Sana na kudai kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mwema na mwenye moyo mkuu, hivyo hawaelewi chanzo cha kuuwawa kwa rafiki yao, nao walidai kuwa wameshangazwa na tukio hilo.

 

Naye Ochieng Geoffrey alisema, ” haki itendeke kwa Emily Chepkemoi ambaye aliuawa nyumbani kwake huko Homabay, kwasababu hilo tukio limewashitua wengi.

Leave A Reply