The House of Favourite Newspapers

Mwanamke akatwa titi gesti

0

Stori: Mwandishi Wetu, UWAZI
KATAVI: Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Zuhura Salum, mkazi wa Mtaa wa Majengo, wilayani Mpanda, Mkoa wa Katavi amejeruhiwa titi la kulia baada ya kukatwa na kisu akiwa gesti.

Mwanamke huyo alijeruhiwa wakiwa wamelala na mpenzi wake katika nyumba ya kulala wageni ya Maridadi mjini Mpanda.Akithibitisha habari hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, ACP Dhahiri Kidavashari (pichani) alisema tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita katika nyumba hiyo ya kulala wageni iliyopo Mtaa wa Majengo.

“Siku ya tukio Zuhura mwenye miaka 34 alikuwa amelala kwenye nyumba hiyo ya wageni akiwa na mpenzi wake aitwaye Iddi Salehe.

“Wakiwa wamelala mtuhumiwa Salehe aliamka na kumvizia Zuhura akiwa usingizini na kumchoma au kumkata kisu kwenye titi lake la kulia hivyo kumjeruhi vibaya,” alisema kamanda huyo.

Aliongeza kuwa, Zuhura alipiga mayowe ya kuomba msaada ambapo walinzi wa gesti hiyo walimsaidia kwa kumkamata mtuhumiwa kisha wakatoa taarifa polisi ambao muda mfupi baadaye walifika na kumtia mbaroni mtuhumiwa.

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika na kujulikana kisa,” alisema Kamanda Kidavashari.

Leave A Reply