The House of Favourite Newspapers

Mwanamke kutokuwa na uwezo wa tendo la ndoa

0

Couple-in-BedTunapozungumzia mwanamke kukosa uwezo wa tendo hili la kujamiiana hapa tunamaanisha anakuwa hana hamu ya tendo hilo au hata akilifanya hafurahii.

Uwezo wa kufanya tendo la kujamiiana kwa mwanamke tunategemea unapungua taratibu kuanzia umri wa miaka hamsini, siyo unaisha ila unaanza kupungua taratibu kadiri umri unavyosonga mbele hadi baadaye unaisha kabisa.

Katika umri huo ndipo tunategemea kusikia mwanamke anaanza kusema hamu ya tendo hilo inapungua au imepungua na hata akilifanya hafurahii kama zamani, hii inatokana na upungufu wa vichocheo muhimu vya ‘Estrogen’ ambavyo ni lazima vipungue katika umri huo ambao mwanamke tayari ameshafikia ukomo wa hedhi na uzazi. Endapo vichocheo hivi vitaendelea kuwa juu katika umri huo au ataviongeza, basi kuna hatari ya mwanamke kupata saratani ya mfuko wa uzazi.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA

Hali ya kutohisi hamu ya tendo na kutopata raha ya tendo ni ya kawaida katika umri mkubwa wa mwanamke kuanzia miaka 50 lakini si ya kawaida katika umri wa chini ya hapo, siyo kawaida kwa mwanamke wa umri wa miaka 20 hadi 48 kupata tatizo hili. Endapo mwanamke wa umri huu atalalamika hali hiyo basi ni tatizo linalohitaji uchunguzi wa kina.

Katika umri wa kuzaa, pale mwanamke anapoendelea kupata siku zake kama kawaida tunategemea mwili wake upo vizuri, homoni zake zinafanya kazi vizuri na anafurahia maisha yake.

Kutohisi hamu ya tendo la ndoa ni kutopata hisia za kimapenzi hata akimuona mwenzi wake, akiguswa au hata akiambiwa maneno ya mapenzi hapati hisia wala msisimko wowote wa kimapenzi.

Mwanamke asiyefurahia tendo la ndoa ni yule asiyefikia kilele cha tendo hilo, mwanamke akifikia kilele hutoa majimaji na huwa na hali ya kumaliza tendo na kupumzika lakini akiwa na tatizo hili hafikii hapo na hufanya tendo hilo basi tu na humridhisha tu mpenzi wake.

CHANZO CHA TATIZO

Tumeona mwanamke kupoteza uwezo wa kufanya tendo la kujamiiana ni kutokuwa na hamu ya tendo na kutofurahia tendo. Tatizo la kutokuwa na hamu ya tendo la kujamiiana huweza kusababishwa na hali ya kutofurahia tendo.

Kutokuwa na hamu hutokana zaidi na tatizo la kisaikolojia endapo mwanamke hayupo vizuri kisaikolojia kama kuna mgogoro wa kimahusiano, kutoandaliwa vizuri kabla ya tendo na kupata maumivu wakati wa tendo.

Mwanamke kutofurahia tendo kutokana na tatizo la kisaikolojia la muda mrefu, maumivu wakati wa tendo, magonjwa sugu kama kisukari, HIV, kansa na mengineyo. Mwanamke anayetumia madawa makali mfano dawa za HIV, kansa, kisukari na nyingine kwa muda mrefu pia hupatwa na tatizo hili. Uchovu wa mwili kutokana na kazi nyingi, uchovu wa akili na kuwa na mawazo mengi kutokana na mambo ya kikazi, kifamilia na kijamii huweza kukufanya upate tatizo hili.

DALILI ZA TATIZO

Mwanamke mwenye tatizo la kutohisi hamu huwa yupo tu na anaweza kukaa muda mrefu hata zaidi ya mwaka bila kufanya tendo hili na hana tatizo lolote, huendelea tu na shughuli zake. Mwenyewe atakuambia labda mwenzake amuanze lakini vinginevyo hajisikii hamu kabisa. Kitaalamu hawezi kupata tatizo lolote kiafya labda kama yupo kwenye uhusiano ndiyo italeta mgogoro.

Mwanamke asiyefurahia tendo anaweza kuwa na historia ya kuwa na maumivu wakati wa tendo, kama alishawahi kuingiliwa kwa nguvu au kama mwenzake yaani mume ana matatizo wakati wa tendo aidha hawezi au hamfikishi mara kwa mara.

Kutofurahia tendo kwa muda mrefu humuathiri mwanamke katika afya yake ya akili na hulifanya kwa kujilazimisha.

Wanawake wengi wenye tatizo hili chanzo huwa ni wanaume kushindwa kumudu tendo hili.

Pamoja na uwepo wa vyanzo ambavyo tayari tumeshaviona.

MATIBABU NA USHAURI

Tatizo hili halina dawa maalumu, jambo la msingi ni kujua chanzo chake na kukitibu.

Uchunguzi utazingatia mambo mbalimbali kutegemea na daktari atakavyoona inafaa.

 

Leave A Reply