The House of Favourite Newspapers

Mwanamuziki Tshala Muana Azikwa Kinshasa Kwa Heshima Viongozi na Wasanii Wahudhuria

0

MWILI wa mwanamuziki maarufu wa DRC, Tshala Muana umezikwa Desemba 23, 2022 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

Tshala, aliyekuwa maarufu kama mama wa taifa na kufahamika pia kama ‘Malkia wa Mutuashi’, alifariki Disemba 10, 2022 baada ya kugua kwa muda mrefu.

Kabla ya kuzikwa mwili wake uliagwa na chama chake cha People’s Party for Reconstruction and Democracy (PPRD), ambacho ni chama cha rais mstaafu, Joseph Kabila, na baadaye ukaagwa katika bungee la taifa.
Maziko yake yamehudhuriwa na viongozi mbalimbli wa kisiasa, serikali na wasanii.

Tshala Muana aliyezaliwa 13 May 1958, Lubumbashi atakumbukwa kwa muziki wake uliomtambulisha Afrika, akiwa na albam takribani 20. Albamu yake ya kwanza yaKangungu aliitoa mwaka 1982 na ya mwisho aliitoa mwaka 2016 iliyoitwa Lunzenze

Wimbo wa Karibu yangu alioutoa mwaka 1988 ulimpa umaarufu zaidi katika nchi za Kenya na Tanzania, kutokana na kuuimba kwa lugha ya kiswahili.

MIILI ya ASKARI WANANDOA ILIVYOZIKWA KWA HESHIMA, RISASI ZAPIGWA ANGANI…

Leave A Reply