The House of Favourite Newspapers

Mwanamme Afariki Ghafla Ndani ya Daladala

0

WASAFIRI waliokuwa wamepanda matatu (daladala) katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, waliingiwa na hofu, baada ya mwanamme mmoja kufa ghafla ndani ya basi hilo.

 

Wasafiri na kondakta walitambua kuwa mwanamme huyo amekufa wakati walipojaribu kumwambia atoe njia kwa msafiri mwenzake ambaye alikuwa anataka kutoka ndani ya gari lakini hakuweza kujibu lolote na alionekana kupoteza fahamu.

 

Maafisa wa wizara ya afya waliitwa katika eneo la tukio baada ya polisi kukataa kusafirisha mwili kwa hofu ya uwezekano kuwa mwanamme huyo alikuwa na maambukizi ya Covid-19.

 

Maafisa waliupulizia dawa mwili wa mwanamme huyo ulipokuwa ndani ya mwili na baadaye waliondoka nao ndani ya mfuko maalum.

Leave A Reply