The House of Favourite Newspapers

Mwandishi Wa Al Jazeera, Samer Abu Daqqa, Afariki Gaza

0
Mwandishi wa habari na Mpiga picha wa Shirika la habari la Al Jazeera, Samer Abu Daqqa

Mwandishi wa habari na Mpiga picha wa Shirika la habari la Al Jazeera, Samer Abu Daqqa aliyejeruhiwa katika shambulio la kombora lililotokea leo huko Gaza,amefariki dunia.

Katika shambulio hilo Mwandishi mwingine ambaye pia ni Mtangazaji wa Al Jazeera Wael Al Dahdouh alijeruhiwa na kupelekwa hospitali.

Shambulio hilo lilitokea katika shule moja ambayo kwa sasa inatumika kama sehemu mojawapo ya kujihifadhi.

Itakumbukwa kuwa takribani mwezi mmoja uliopita Dahdouh alipoteza familia yake ,akiwemo mke wake, watoto wake wawili pamoja na mjukuu wake kwenye shambulio lingine.

Leave A Reply