The House of Favourite Newspapers

Mwanza Yazizima Kuagwa Mwili wa Hayati Magufuli – Video

0

WAKAZI wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani,wamejitokeza kuuaga mwili wa Hayati Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba na katika barabara ambazo amepita,huku shughuli zote zikisimama na maduka yakiwa yamefungwa kwa siku nzima.

 

Wakazi hao waliojawa simanzi waliupamba msafara huo kwa majani ya miti ya mitende,wengine walitandika nguo zao katika barabara uliopita mwili na kumwaga maji,huku vilio vikitawala kwa watu walika zote.

 

Akitoa salamu za pole kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani,waziri mkuu Kassim Majaliwa alisema,Hayati Magufuli ameacha alama katika Taifa la Tanzania ambazo ni amani upendo na mshikamano na miradi ambayo ni kioo kikubwa cha nchi.

 

“Mwanza ni sehemu ya kihistoria kwa Hayati Magufuli,kwani ndiko alizaliwa na kulelewa,kusomea na kazi alianzia hapa,hivyo tuendelee kuwa watulivu na shughuli hii ifanyike kwa amani hadi tutakapo mweka kwenye nyumba yake ya milele,tunashukuru sana kwa utulivu na mapokezi mazuri kwa wana Mwanza,” alisema Majaliwa.

 

Aidha Majaliwa alitoa salamu za pole kwa wananchi,ambazo alitumwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kuwa,”anawaomba Watanzania wawe watulivu,kushikamana,kuwa na subila ili waendelee kulijenga Taifa na kuyaenzi yale aliyoyaacha hayati Magufuli.

 

“Tunawashukuru waandishi wa habari na vyombo yao kwa kutoa mchango mkubwa wa kutoa taarifa kwa wananchi wa ndani na nje,kiukweli waendelea kufanya kazi nzuri sisi serikali tunapata moyo na kuendelea kuithamini sekta ya habari,” alisema Majaliwa.

 

Katika shughuli hiyo Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Hamed Suiman Abdarah,aliongoza wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani kuuaga mwili wa Hayati John Magufuli,katika uwanja wa CCM Kirumba.

 

Naye waziri wa Ofisi ya waziri mkuu kazi vija na ajira Jenista Mhagama,alisema wametekeleza maagizo na majukumu toka walivyoanza shughuli hiyo,hivyo inahitaji moyo na uvumilivu mkubwa na wataendelea kutekeleza kwa heshima ya juu hadi watakapo mpumzisha katika nyumba ya milele hayati Magufuli.

 

Gazeti hili lilizungumza na wananchi juu ya msiba huu,wengi wao walielekeza kilio chao kwa Rais wa sasa Samia Hassan Suluhu kwani ndiyo aliyebeba hatima ya Taifa hili,hivyo wanamuomba alinde heshima ya Hayati Magufuli.

 

“Hatuna cha kufanya inatubidi tukubaliane na jambo hili, ambalo limetuumiza watanzania na watu wote wa Dunia nzima, hivyo tuma muomba Rais wetu mama yetu tunaimani naye atatufuta machozi kwa kuliweka Taifa kama alivyoliweka Hayati Rais Magufuli katika mikono salama.

 

Na Leah Marco, Mwanza

Leave A Reply