The House of Favourite Newspapers

MWARABU: Kufukuzwa WCB, Diamond Alinipigia Simu – Video

ULE utata kuhusu Kufukuzwa kundini kwa Baunsa wa Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, anayefahamika kwa jina la Mwarabu Fighter, unazidi kuchanganya Watanzania na Mashabiki kwa ujumla.

 

Global TV imekutana USO kwa USO na Mwarabu usiku wa Agosti 23, katika ukumbi wa Samaki Samaki uliopo Masaki kwenye ‘Birthday Party’ ya DJ wa Diamond anayeitwa Rommy Jones na tumepiga nae stori kwa mara nyingine tena kuhusiana na utata huo.

 

Mwarabu amesema hajapewa taarifa rasmi kuwa amefukuzwa WCB isipokuwa menejimenti inamwambia aendelee kusubiri kwahiyo anachokifanya sasa in kupiga mishe zake binafsi na kuendelea kampuni yake ya ulinzi ili maisha yazidi kusonga mbele.

 

Kuhusu kuwasiliana na Diamond, Mwarabu amesema amekuwa akiongea nae sana kwenye simu lakini hata yeye hajamtamkia kuwa arudi kuendelea na kazi.

 

VIDEO: MSIKIE MWARABU AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.