The House of Favourite Newspapers

Mwigulu Aivaa TFF, Simba Kutolewa Ligi ya Mabingwa

0

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amesema Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF halina mipangilio inayoeleweka kimichezo hali iliyopelekea kushindwa kwa vilabu vyetu kufanya vyema katika michuano ya kimataifa.

 

Nchemba ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 22, wakati wakupitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022 nakuitaja moja ya sababu iliyosababishwa na TFF na kupelekea timu ya Simba kushindwa kimataifa kufuatia bodi ya Ligi kuiwekea mechi ya watani wa jadi ikiwa ni siku chache kabla ya kuivaa Kaizer Chiefs ambayo mnyama alitembezewa kichapo cha magoli 4-0.

”Kwa mimi ninavyoangalia kwa jinsi nilivyoiangalia Simba, ilikuwa na uwezo wa kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu.”

 

”Kuna mahali tumekosea, na tunakosea pale ambapo hatuweki vipaumbele, yani sisi mambo yote yapo sawa tu,kwamba mtu anaenda kucheza mchezo ambao unaweza kuleta kombe Tanzania kwa mara ya kwanza, kati kati yake unaenda kuwawekea mchezo mkubwa wa watani wa jadi.”

 

”Simba imeenda kucheza mchezo mkubwa Afrika Kusini bila Game Plan, wenyewe walikuwa wanawaza mechi ya watani wa jadi, hatukuwa na mpango.”

 

”Wapo watu wanalaumu eti Simba kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa eti ilihujumiwa na Senzo Mazingiza, kweli Yanga ambayo imewapa Benard Morrison tena hata nauli waliyomtumia kumleta hapa nchini hamjamlipia kweli iwahujumu dhidi ya Kaizer Chiefs, Kweli Simba iliyoifunga Al Ahly ije ihujumiwe na Senzo na mashabiki wa Yanga”?

 

”Timu zinazokwenda kwenye michuano ya kimataifa, zinaliletea sifa Taifa lazima bodi hizi zinazosimamia lazima wawape vipaumbele.”Ameongeza Waziri Nchemba.

 

Leave A Reply